ROBO FAINALI YA MOTO MBWENI

JKT Tanzania leo wanatarajiwa kuvaana na Young Africans SC katika mchezo wa robo fainali ya CRDB Federation Cup.Mchezo huo utapigwa katika Uwanja wa Meja General Isamuyo Stadium jijini Dar es Salaam majira ya saa 12:30 jioni.
Mchezo huo unatajwa kuwa mgumu kwa upande wa Yanga kutokana na ubora ambao JKT Tanzania wamekuwa nao katika kipindi cha hivi karibuni, huku Yanga pia wakionekana kuwa na wakati mgumu kupata matokeo mazuri wanapocheza kwenye dimba hilo la Mbweni.
Mashabiki wengi wa soka Tanzania wanatarajia ushindani mkubwa katika pambano hilo huku timu zote zikisaka nafasi ya kutinga hatua ya nusu fainali ya michuano hiyo.






