Mtangazaji wa Wasafi FM na mwanachama wa Yanga, Haji Manara, ametoa onyo kali kwa klabu yake kufuatia kupoteza fainali ya Muungano dhidi ya Simba SC. Manara amekosoa tabia ya kujiamini kupiliza na dharau iliyoonyeshwa na upande wa Yanga kabla ya mchezo, akisisitiza kuwa dabi haihitaji mbwembwe za nje ya uwanja bali maandalizi ya dhati. Ameonya kuwa kama nidhamu haitatawala, Yanga inaweza kukumbana na kipigo kingine Jumapili ijayo katika mchezo wa Ligi Kuu.
”Ndio football but na Sisi tupunguze midomo midomo, tunachonga mno kupitiliza wakati kocha wetu ni Muomba Mungu tu!! Tulionyesha kujiamini kupitiliza nje ya uwanja na kufanya mbwembwe nyingi za kipuuzi, Show za kindezi kibao kabla ya mechi tukasahau uzito wa kukutana na Makolo. Derby haihitaji dharau na tusipokuwa makini watatukanda tena Jumapili!! Na Wallah Wakishinda ntakuja na viboko hapo Kaunda kuwatandika.”
