Close Menu
    Facebook X (Twitter) Instagram
    Facebook X (Twitter) Instagram
    SOKALEO
    • HOME
    • KITAIFA
    • KIMATAIFA
    • TETESI ZA SOKA
    • MAGAZETI YA LEO
    • FORUM
    • BOXING
    SOKALEO
    Home » HANS RADAEL: YANGA INAHITAJI MABORESHO MAKUBWA SANA
    Habari za Michezo

    HANS RADAEL: YANGA INAHITAJI MABORESHO MAKUBWA SANA

    ChikaoBy ChikaoApril 30, 202602 Mins Read
    Share Facebook Twitter Pinterest LinkedIn Tumblr Email
    Share
    WhatsApp Facebook Telegram Twitter Pinterest Email
    Mchambuzi wa soka Hans Rafael ametoa tahadhari nzito kwa klabu ya Yanga, akidai kuwa ubora na utawala waliokuwa nao misimu miwili iliyopita sasa umepotea. Hans ameeleza kuwa Simba imefanikiwa kufuta pengo la kiufundi lililokuwepo, jambo linalothibitishwa na Simba kuibuka mbabe katika dabi mbili mfululizo. Amesititiza kuwa Yanga ya sasa inahitaji ujenzi mpya na maboresho makubwa kwani haina tena ule upambanaji na “quality” iliyokuwa ikiwapa kiburi mashabiki wao.
    ​Hans Rafael ameandika hivi:
    ​”Miaka miwili au mitatu iliyopita Yanga walikuwa na timu nzuri sana, walikuwa na kikosi bora sana, ndio maana kila kitu kilikuwa rahisi kwao, kila kocha alionekana bora na walitengeneza “Gape” kubwa baina yao na Simba ndio maana walishinda dabi 6 mfululizo.
    ​Ila ukitazama sasa mambo yamebadilika, dabi mbili mfululizo Simba anaibuka mbabe siyo kwa bahati mbaya kuna mawili Simba wameimarika zaidi au Yanga wameshuka (hawana timu).
    ​Lile gape kubwa halipo tena, ile quality ya Yanga kwenye mpira haionekani, ule upambanaji wa Yanga umepungua…..mfano jana una struggle kupata mchezaji wa Yanga aliyekuwa na woow! performance.
    ​Mwishoni mwa msimu hii timu inahitaji maboresho makubwa sana, hata kama itashinda ubingwa wa ligi ila Yanga hii siyo ya misimu mitatu au miwili iliyopita…..Ujenzi mpya unahitajika.
    ​Ni jambo la kujua nyakati na kuondoa mazoea Yanga hii haikupi tena kiburi cha kusimama na kusema Simba atakufa…..hii siyo ile Yanga ya Aziz Ki, Aucho na Mayele.
    ​Gape baina yao na Simba limeondoka, ujenzi mpya unahitajika
    Share. Facebook Twitter Pinterest LinkedIn Tumblr Email
    Previous ArticleMECHI NA SIMBA ILIKUWA YA KIRAFIKI
    Next Article HAJI MANARA AIJIA JUU YANGA, ASEMA ATAWACHAPA VIBOKO

    Related Posts

    HAJI MANARA AIJIA JUU YANGA, ASEMA ATAWACHAPA VIBOKO

    April 30, 2026

    MECHI NA SIMBA ILIKUWA YA KIRAFIKI

    April 30, 2026

    Mshindi lazima apatikane leo Yanga SC vs Simba SC, Muungano CUP

    April 29, 2026
    Add A Comment
    Leave A Reply Cancel Reply

    LATEST POSTS

    HAJI MANARA AIJIA JUU YANGA, ASEMA ATAWACHAPA VIBOKO

    HANS RADAEL: YANGA INAHITAJI MABORESHO MAKUBWA SANA

    MECHI NA SIMBA ILIKUWA YA KIRAFIKI

    Wafungaji Bora Mapinduzi Cup 2026

    Mshindi lazima apatikane leo Yanga SC vs Simba SC, Muungano CUP

    IBENGE AKIRI KUTORIDHISHWA NA KIWANGO CHA WACHEZAJI WAKE

    matokeo ya Azam FC vs Yanga SC Leo 25/04/2026

    © 2026 SOKALEO TANZANIA | All Rights Are Reserved

    Type above and press Enter to search. Press Esc to cancel.