Klabu ya Yanga SC imezua taharuki katika soko la usajili barani Afrika baada ya kuripotiwa kugomea ofa mbili nono kutoka kwa vigogo wa soka la Kaskazini, Zamalek ya Misri na CR Belouizdad ya Algeria, zilizokuwa zikimhitaji mlinda mlango wao namba moja, Djigui Diarra.
Matajiri hao wa Kiarabu wamevutiwa na kiwango cha hali ya juu alichokionyesha kipa huyo mwenye umri wa miaka 30 kwenye michuano ya AFCON 2025 nchini Morocco, ambapo alikuwa mhimili mkuu wa timu ya taifa ya Mali kabla ya kutolewa katika hatua ya robo fainali.
Licha ya ofa hizo kutajwa kuwa na thamani kubwa, uongozi wa Yanga umetoa jibu la mkato la “Diarra is not for sale” (Diarra hauzwi), ukisisitiza kuwa kipa huyo bado ana mkataba wa kudumu mpaka mwaka 2027.
Hatua hii inatafsiriwa kama mkakati wa Yanga kulinda heshima yake na kuimarisha kikosi kuelekea hatua muhimu za Ligi ya Mabingwa Afrika (CAFCL), huku wakituma salamu kwa wapinzani wao kuwa “Screen Protector” huyo ni sehemu ya mipango yao ya muda mrefu na haitashawishika na fedha yoyote kumpoteza kipa huyo katikati ya msimu.










Leave a Reply