Close Menu
    Facebook X (Twitter) Instagram
    Facebook X (Twitter) Instagram
    SOKALEO
    • HOME
    • KITAIFA
    • KIMATAIFA
    • TETESI ZA SOKA
    • MAGAZETI YA LEO
    • FORUM
    • BOXING
    SOKALEO
    Home » Kocha wa Simba Ahaidi Makubwa, Kazi Inaanza Mapinduzi Cup
    KITAIFA

    Kocha wa Simba Ahaidi Makubwa, Kazi Inaanza Mapinduzi Cup

    ChikaoBy ChikaoJanuary 3, 202602 Mins Read
    Share Facebook Twitter Pinterest LinkedIn Tumblr Email
    Kocha simba
    Share
    WhatsApp Facebook Telegram Twitter Pinterest Email

    KOCHA wa Klabu ya Simba, Steve Barker, amesema kuwa mchezo wa kesho dhidi ya Muembe Makumbi katika Kombe la Mapinduzi ni muhimu kwa maandalizi ya kikosi chake.

    Amesema  licha ya kuelewa kuwa mashindano hayo yana uzito mkubwa kama ilivyo kwa mashindano ya kimataifa yanayowakabili baadaye.

    Barker amesema lengo kubwa la Simba katika michuano hiyo ni kuwapa wachezaji muda wa kucheza na kurejesha ubora wao wa ushindani baada ya mapumziko, huku akitumia fursa hiyo kujaribu mbinu mbalimbali kabla ya mechi ngumu zijazo.

    Barker ameongeza  kuwa ingawa Kombe la Mapinduzi  kipaumbele kikubwa kwa Simba, bado anaamini ni jukwaa zuri la kuwakagua wachezaji wake na kuona kiwango chao cha utayari, hasa wale waliokuwa nje ya uwanja kwa muda kutokana na majeraha au majukumu mengine.

    Kocha huyo amesema anafurahi kuona ari na morali ya wachezaji wake ipo juu,  kila mchezaji anaonesha njaa ya ushindani na dhamira ya kupigania nafasi ndani ya kikosi cha kwanza kuelekea mechi muhimu za Ligi ya Mabingwa Afrika (CAF Champions League).

    “Lengo letu si tu kushinda mechi, bali kuona namna wachezaji wanavyotekeleza maelekezo ya kiufundi ndani ya uwanja, kujenga maelewano na kuongeza kasi ya timu,” amesema Barker.

    Akizungumzia mchezo dhidi ya Muembe Makumbi, Barker amesema ana heshima kubwa kwa mpinzani wao na ameandaa kikosi chake kucheza kwa umakini mkubwa.

    Amesema  katika soka hakuna mechi nyepesi na kila mpinzani anapaswa kuchukuliwa kwa uzito unaostahili.

    Simba inatarajia kushuka dimbani kesho ikiwa na dhamira ya kuonyesha ubora wake, huku mashabiki wakitarajia kuona mabadiliko chanya katika uchezaji wa timu yao kuelekea safari ya Ligi ya Mabingwa Afrika.

    Share. Facebook Twitter Pinterest LinkedIn Tumblr Email
    Previous ArticleMsiichukulie Poa Simba ya Sasa, Mazito Yatajwa
    Next Article Je sababu zilizopelekea kuachana nao hazipo tena? – Wilson Oruma

    Related Posts

    WANA SIMBA WASIFEDHESHWE, TUNAJUA NAMNA YA KUPUNGUZA POINTI

    April 12, 2026

    SIMBA YAANZA USAJILI NA MIPANGO YA UWANJA MPYA BUNJU

    April 8, 2026

    SURE BOY HATIMAE AOMBA KUSEPA YANGA

    April 8, 2026
    Add A Comment
    Leave A Reply Cancel Reply

    LATEST POSTS

    WANA SIMBA WASIFEDHESHWE, TUNAJUA NAMNA YA KUPUNGUZA POINTI

    SIMBA YAANZA USAJILI NA MIPANGO YA UWANJA MPYA BUNJU

    SURE BOY HATIMAE AOMBA KUSEPA YANGA

    HATIMAE MIGUU IMEANZA KUMSALITI CHAMA

    AFCON EAST AFRICA TAREHE YATANGAZWA

    MPANZU NA FEI TOTO WAKUTANA USO KWA USO KWENYE VITA YA ASSIST

    IBENGE ATANGAZA VITA JUU YA KIKOSI CHA SIMBA

    © 2026 SOKALEO TANZANIA | All Rights Are Reserved

    Type above and press Enter to search. Press Esc to cancel.