Rais Karia Amtimbia Gamondi Mazoezini, Amkumbusha Haya

Rais wa TFF, Wallace Karia ametembelea mazoezi ya Timu ya Taifa @Taifastars_ inayojiandaa na mchezo wa kirafiki kwenye kalenda ya FIFA dhidi ya Kuwait utakaochezwa Novemba 15,2025 Nchini Misri.

Taifa Stars ambao wameingia kambini siku ya jana wanafanya mazoezi katika dimba la Gymkhana kabla ya kusafiri kuelekea Nchini Misri kwa ajili ya mchezo huo.