Taarifa zinaeleza kuwa Senzo Mazingiza, aliyewahi kuwa Mtendaji Mkuu (CEO) wa vilabu vikubwa vya Tanzania — Simba SC na Yanga SC, anatarajiwa kujiunga na TRA Sports Club kama CEO mpya wa klabu hiyo.
Senzo anatajwa kupewa jukumu la kuboresha mfumo wa uendeshaji wa klabu hiyo, kuijenga katika misingi imara ya kisasa ya soka, na kuhakikisha TRA Sports Club inakuwa miongoni mwa timu bora nchini katika miaka ijayo.
Kama akiteuliwa rasmi, itakuwa ni hatua nyingine kubwa kwa Senzo, ambaye amejizolea sifa kubwa katika usimamizi wa soka la Afrika Mashariki.










Leave a Reply