Klabu ya Young Africans SC (Yanga) inadaiwa kuanza mazungumzo ya awali na winga wa Singida Black Stars, Lamin Jarjou, kwa lengo la kumsajili kuelekea msimu wa 2026/27 kufuatia kiwango kizuri alichoonyesha katika Ligi Kuu msimu huu.
Jarjou amekuwa chaguo la kwanza kikosini humo, akimuweka benchi Offen Chikola ambaye yupo Singida kwa mkopo akitokea Yanga. Hadi sasa, Jarjou amechangia bao moja na asisti tatu, huku taarifa zikieleza kuwa mazungumzo kati ya pande hizo mbili yanaendelea vyema na huenda yakafikia hatua nzuri hivi karibuni.
