Mabingwa wa Afrika, Senegal wamepokonywa rasmi taji la Africa Cup of Nations miezi miwili baada ya sherehe kubwa za ushindi, kufuatia uamuzi wa kushangaza wa Shirikisho la Soka Afrika (CAF).
Uamuzi huo umeipa Morocco ushindi wa mezani wa mabao 3-0, baada ya bodi ya rufaa ya CAF kukubaliana na malalamiko ya Morocco kuhusu tukio la fainali iliyochezwa Rabat Januari 18.
CHANZO CHA MGOGORO
Katika dakika za mwisho za mchezo: Mwamuzi Jean Jacques Ndala alitoa penalti kwa Morocco baada ya VAR kubaini faulo ya El Hadji Malick Diouf dhidi ya Brahim Díaz
Senegal walikuwa tayari na hasira baada ya bao la Ismaïla Sarr kufutwa
Kocha wa Senegal Pape Thiaw aliwaamuru wachezaji wake kuondoka uwanjani kupinga maamuzi hayo.
Hata hivyo, Sadio Mané alijaribu kuwazuia na kuwataka warudi kuendelea na mchezo.
KILICHOAMULIWA NA CAF
CAF imesema wazi kuwa:
-Senegal walivunja sheria kwa kukataa kuendelea na mchezo
-Mechi ilipaswa kuhesabika kuisha pale walipotoka uwanjani
-Hivyo, ushindi umetolewa kwa Morocco kwa mabao 3-0
ADHABU NA MATOKEO
Kocha Pape Thiaw amefungiwa mechi 5 na kutozwa faini ya dola 100,000
Wachezaji kadhaa akiwemo Iliman Ndiaye na Achraf Hakimi wamepewa adhabu
Rais wa FIFA Gianni Infantino alilaani tukio hilo akilitaja kama “lisilokubalika”
MSIMAMO WA MOROCCO
Shirikisho la soka la Morocco limesema:
Lengo lao halikuwa kupinga uwezo wa timu bali kuhakikisha sheria za mashindano zinaheshimiwa.
