Close Menu
    Facebook X (Twitter) Instagram
    Facebook X (Twitter) Instagram
    SOKALEO
    • HOME
    • KITAIFA
    • KIMATAIFA
    • TETESI ZA SOKA
    • MAGAZETI YA LEO
    • FORUM
    • BOXING
    SOKALEO
    Home » MAJERUHI YATIKISA SIMBA, NANGU KURUDI JULAI
    KITAIFA

    MAJERUHI YATIKISA SIMBA, NANGU KURUDI JULAI

    ChikaoBy ChikaoMarch 15, 202602 Mins Read
    Share Facebook Twitter Pinterest LinkedIn Tumblr Email
    Share
    WhatsApp Facebook Telegram Twitter Pinterest Email

    UONGOZI wa klabu ya Simba SC umeweka wazi hali ya wachezaji wake waliopo majeruhi, huku beki Wilson Nangu akitarajiwa kurejea uwanjani Julai mwaka huu baada ya kuendelea na matibabu.

    Akizungumza kuhusu hali ya kikosi, Meneja wa Idara ya Habari na Mawasiliano wa Simba, Ahmed Ally amesema wachezaji wote walioumia wanaendelea na matibabu yao chini ya uangalizi wa madaktari wa timu, wakifuata maelekezo maalum ili kuhakikisha wanarejea wakiwa katika hali nzuri.

    Alifafanua kuwa Nangu alifanyiwa upasuaji baada ya kupata majeraha makubwa na kwa sasa amewekewa P.O.P, hatua ambayo ni sehemu ya mchakato wa matibabu yake.

    Baada ya hapo atawekewa bao maalum ambalo atalivaa kwa muda hadi pale atakapokuwa tayari kuanza mazoezi tena.

    Ahmed amesema kwa sasa mchezaji huyo amerudi nyumbani kwao Boma Ng’ombe, Kilimanjaro kwa ajili ya kupata utulivu na kuendelea na hatua za kupona.

    “Ripoti za madaktari zikionyesha kuwa anaweza kuanza mazoezi mwezi Julai endapo maendeleo yake yataendelea kuwa mazuri,” amessma.

    Mbali na Nangu, Ahmed ameongeza kuwa wachezaji wengine wanaosumbuliwa na majeraha ni pamoja na Abdulrazack Hamza, Moussa Camara na Yakubu Suleiman ambao nao bado wanaendelea na matibabu na wanatarajiwa kukaa nje ya uwanja kwa muda hadi watakapopata nafuu kamili.

    Amesema uongozi wa Simba umeendelea kuwahakikishia mashabiki kuwa unafuatilia kwa karibu maendeleo ya wachezaji hao ili kuhakikisha wanarejea uwanjani wakiwa tayari kusaidia timu kufikia malengo yake ya msimu.

    Share. Facebook Twitter Pinterest LinkedIn Tumblr Email
    Previous ArticleVINARA LIGI DARAJA LA KWANZA RAHA TUPU

    Related Posts

    VINARA LIGI DARAJA LA KWANZA RAHA TUPU

    March 15, 2026

    BAJABER ARUDI KWENYE RAMANI KUPITIA WITO WA TAIFA

    March 15, 2026

    YANGA WAINGIA UWANJA WA MKAPA WAKIWA NA MIKAKATI YA KUIFUNGA AZAM FC

    March 15, 2026
    Add A Comment
    Leave A Reply Cancel Reply

    LATEST POSTS

    MAJERUHI YATIKISA SIMBA, NANGU KURUDI JULAI

    VINARA LIGI DARAJA LA KWANZA RAHA TUPU

    “Reece James ni beki bora zaidi wa kulia Duniani”-Rosenior.

    BAJABER ARUDI KWENYE RAMANI KUPITIA WITO WA TAIFA

    YANGA WAINGIA UWANJA WA MKAPA WAKIWA NA MIKAKATI YA KUIFUNGA AZAM FC

    Tanzania Yatoa Zaidi ya Sh80 Bilioni CAF Ili Kuwa Mwenyeji wa AFCON 2027

    Bilioni Zatengwa 388.8 Kujenga AFCON City Unguja

    © 2026 SOKALEO TANZANIA | All Rights Are Reserved

    Type above and press Enter to search. Press Esc to cancel.