Ruka hadi maudhui
SOKALEO

HAWA HAPA WACHEZAJI WA TAIFA STARS WALIO NA MAJERAHA

Chikao
HAWA HAPA WACHEZAJI WA TAIFA STARS WALIO NA MAJERAHA

Timu ya Taifa ya Tanzania national football team imepata pigo kubwa katika safu yake ya ulinzi baada ya mabeki wake watatu kupata majeraha makubwa yaliyowalazimu kufanyiwa upasuaji, hali itakayowafanya kukaa nje ya uwanja hadi mwishoni mwa msimu wa 2025/26.

Mabeki waliopata majeraha hayo ni Wilson Nango wa Simba SC, Dikson Job wa Young Africans S.C. pamoja na Abdulrazack Hamza ambaye pia anakipiga katika klabu ya Simba SC. Kukosekana kwa mabeki hao kunatajwa kuwa pengo kubwa kwa kikosi cha Taifa Stars kuelekea mechi zake zijazo.

Kutokana na hali hiyo, kocha wa Taifa Stars Miguel Gamondi atalazimika kutafuta mbadala katika safu ya ulinzi, ambapo macho yake yanaelekezwa zaidi kwa mabeki wa Yanga Ibrahim Bacca na Bakari Mwamnyeto ili kuimarisha eneo hilo muhimu la ulinzi wa timu ya taifa.

Shiriki:

Habari Zinazohusiana

Zaidi →

Kocha wa Simba Steve Barker Awasha Moto Mpya

YAMAL: Afikisha mchango wa mabao 20 ndani ya mechi 13