Close Menu
    Facebook X (Twitter) Instagram
    Facebook X (Twitter) Instagram
    SOKALEO
    • HOME
    • KITAIFA
    • KIMATAIFA
    • TETESI ZA SOKA
    • MAGAZETI YA LEO
    • FORUM
    • BOXING
    SOKALEO
    Home » Msiichukulie Poa Simba ya Sasa, Mazito Yatajwa
    KITAIFA

    Msiichukulie Poa Simba ya Sasa, Mazito Yatajwa

    ChikaoBy ChikaoJanuary 2, 202602 Mins Read
    Share Facebook Twitter Pinterest LinkedIn Tumblr Email
    simba
    Share
    WhatsApp Facebook Telegram Twitter Pinterest Email

    MENEJA wa timu ya Simba, Patrick Rweyemamu amesema hakuna sababu ya wapinzani kuwachukulia poa Wekundu wa Msimbazi licha ya kwenda Visiwani Zanzibar.

    Amesema  kikosi chenye wachezaji pungufu,  timu hiyo imejipanga kuonyesha ubora wake katika michuano ya Kombe la Mapinduzi.

    Simba kwa sasa wapo Visiwani Zanzibar tayari kwa ajili ya kushiriki michuano hiyo ya kihistoria, ambapo wanatarajiwa kushuka dimbani kesho Januari 3 kucheza mchezo wao wa kwanza dhidi ya Muembe Makumbi City, New Amaan Complex.

    Rweyemamu amesema licha ya kikosi hicho kuwa na mchanganyiko wa wachezaji wa kikosi cha kwanza na chipukizi kutoka timu ya vijana, dhamira ya Simba imebaki ileile ya kushindana kwa nguvu zote na kupambania matokeo chanya katika kila mchezo.

    Ameeleza kuwa baadhi ya wachezaji wao muhimu hawakuwepo kutokana na majukumu ya timu ya Taifa, lakini hilo halijapunguza ari ya kikosi, kwani maandalizi yamefanyika kwa umakini mkubwa kuhakikisha wanatimiza malengo yao.

    “Hatujaja na kikosi kamili kwa sababu wachezaji wengi wapo kwenye timu ya Taifa, lakini tumepanga vizuri na tumekuja kuonyesha kuwa tunahitaji kulichukua kombe hili,” alisema Rweyemamu.

    Meneja huyo ameongeza kuwa timu imeweka mikakati madhubuti kuhakikisha inafikia malengo yake, ikiwemo kupambana kwa nidhamu, kujituma uwanjani na kulinda heshima ya klabu katika mashindano hayo.

    Amesisitiza pia kuwa michuano hiyo ni fursa muhimu kwa kocha mpya wa Simba, Steve Barker, kupata nafasi ya kuliona na kulitathmini kikosi chake kwa karibu, jambo litakalompa mwanga wa kiufundi kuelekea changamoto zijazo za msimu.

    Simba SC
    Share. Facebook Twitter Pinterest LinkedIn Tumblr Email
    Previous ArticleRasmi Clatous Chama Atibitisha Kurejea Simba
    Next Article Kocha wa Simba Ahaidi Makubwa, Kazi Inaanza Mapinduzi Cup

    Related Posts

    WANA SIMBA WASIFEDHESHWE, TUNAJUA NAMNA YA KUPUNGUZA POINTI

    April 12, 2026

    SIMBA YAANZA USAJILI NA MIPANGO YA UWANJA MPYA BUNJU

    April 8, 2026

    SURE BOY HATIMAE AOMBA KUSEPA YANGA

    April 8, 2026
    Add A Comment
    Leave A Reply Cancel Reply

    LATEST POSTS

    WANA SIMBA WASIFEDHESHWE, TUNAJUA NAMNA YA KUPUNGUZA POINTI

    SIMBA YAANZA USAJILI NA MIPANGO YA UWANJA MPYA BUNJU

    SURE BOY HATIMAE AOMBA KUSEPA YANGA

    HATIMAE MIGUU IMEANZA KUMSALITI CHAMA

    AFCON EAST AFRICA TAREHE YATANGAZWA

    MPANZU NA FEI TOTO WAKUTANA USO KWA USO KWENYE VITA YA ASSIST

    IBENGE ATANGAZA VITA JUU YA KIKOSI CHA SIMBA

    © 2026 SOKALEO TANZANIA | All Rights Are Reserved

    Type above and press Enter to search. Press Esc to cancel.