Ruka hadi maudhui
SOKALEO

Kauli ya Ibwe Kuhusu Kimataifa ni Balaa, Hao wa Kariakoo Bado Sana

Chikao
Kauli ya Ibwe Kuhusu Kimataifa ni Balaa, Hao wa Kariakoo Bado Sana
Msemaji na Afisa Habari wa Azam FC, Hashim Ibwe, ameeleza kujiamini kwa klabu yake kuelekea michuano ya kimataifa ya Kombe la Shirikisho Barani Afrika (CAF Confederation Cup), akibainisha kuwa klabu hiyo inaanzia michezo yake raundi ya pili kwa sababu ni timu kubwa.
Ibwe pia alizungumzia uamuzi wa Yanga SC kutumia Uwanja wa Azam Complex (Chamazi) kwa mchezo wao wa marudiano, akifafanua kuwa Azam FC haina shida kuwapokea kwa kuwa ni fursa ya kibiashara ya kupata mapato, ingawa masimango ya uwanjani yatafuata mara baada ya mchezo huo kumalizika.
​Akiipongeza klabu ya Singida Black Stars kwa ushindi mnono waliopata ugenini, Ibwe alikiri kuwa matokeo hayo yameiachia Azam FC deni kubwa la kufanya vizuri zaidi ili kuiwakilisha nchi vyema katika michuano hiyo ya kimataifa.
Alikumbusha kuwa Azam FC ndiyo timu iliyovuna alama nyingi zaidi msimu uliopita kwenye michuano ya kimataifa, hivyo kiwango kilichoonyeshwa na Singida kinaongeza hamasa na kuthibitisha ubora wa wawakilishi wa Tanzania katika Kombe la Shirikisho.
​Aidha, Ibwe alieleza kuwa benchi la ufundi chini ya kocha Florent Ibenge linaendelea kufanya tathmini na kuwasoma kwa umakini wapinzani wao watakaokutana nao ili kutorudia makosa na kuhakikisha wanatinga hatua ya makundi. Alihitimisha kwa kusisitiza kuwa kikosi chao kina upana mkubwa wa wachezaji na kila mmoja yupo tayari kujituma kwa asilimia mia moja ili kupata matokeo chanya na kutowaangusha mashabiki wa klabu hiyo.
Shiriki:

Habari Zinazohusiana

Zaidi →