MAKUBWA!! UWEPO WA ABRAHAM MORICE WAZUA BALAA HILI SIMBA

Abraham Morice

UONGOZI wa Simba SC umeweka wazi kuwa unajivunia uwepo wa kiungo mshambuliaji Abraham Morice kutokana na kazi kubwa anayofanya kwenye mechi za ushindani.

Nyota huyo amekuwa kwenye ubora katika mechi ambazo anapata nafasi ya kucheza akianzia benchi ama kikosi cha kwanza amekuwa akionyesha kitu.

Katika mchezo wa Ligi Kuu Bara ya NBC dhidi ya JKT Tanzania uliochezwa Novemba 8,2025 alitoa pasi ya bao kwa Jonathan Sowah alipoanzia benchi.

Wachezaji hao wote wawili kwenye mchezo huo walianzia benchi na mwisho ubao ulisoma JKT Tanzania 1-2 Simba SC walipovuna pointi tatu muhimu.

Ahmed Ally, Meneja wa Idara ya Habari na Mawasiliano Simba SC amesema kuwa wanatambua umuhimu wa kila mchezaji katika kikosi huku Morice akiwa na pasi za mpenyezo.

“Abraham Morice amekuwa akifanya vizuri kwenye mechi ambazo anacheza, iwe anaanzia benchi ama kuanza kikosi cha kwanza. Katika mchezo wetu dhidi ya JKT Tanzania alianzia benchi na alipoingia alikuwa kwenye ubora katika pasi na mikimbio.Ametoa pasi ya bao kwa Simba Mweusi Jonathan Sowah hii ni kazi kubwa kwelikweli tunajivunia uwepo wake,”.