Home KITAIFA AZAM FC KUANZA KAZI LEO RWANDA MECHI DHIDI YA APR FC

AZAM FC KUANZA KAZI LEO RWANDA MECHI DHIDI YA APR FC

185
0
azam

AZAM FC wakiwa nchini Rwanda ambapo wameweka kambi wanatarajiwa kushiriki michuano ya Inkera Y’abahizi baada ya kualikwa na wenyeji wao APR FC na leo Agosti 19 2025 watakuwa na kibarua kuhesabu mechi nne za ushindani.

Ipo wazi kwamba Azam FC inapeperusha bendera ya Tanzania kwenye anga la kimataifa ikiwa ni katika Kombe la Shirikisho na inashiriki Ligi Kuu Tanzania Bara ya NBC ambayo ni namba nne kwa ubora Afrika.

Leo Azam FC inatarajiwa kucheza na Police FC, mechi ya pili itakuwa dhidi ya AS Kigali Agosti 21, watakutana na wenyeji APR, Agosti 24 2025.

Advertisement

Kete ya nne kukamilisha dakika 360 kwa Azam FC inayonolewa na Kocha Mkuu, Florent Ibenge inatarajiwa kuwa dhidi Vipers ya Uganda Agosti 29 2025.

Timu hiyo imefanya usajili mkubwa kuelekea msimu mpya wa 2025/26 unaotarajiwa kuwa na ushindani mkubwa. Miongoni mwa wachezaji waliopo katika kikosi hicho ni Sadio Kanoute ambaye aliwahi kucheza Simba SC, Fofana ambaye ni kipa na Barakat hawa wote wamesaini dili la miaka miwili.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here