Close Menu
    Facebook X (Twitter) Instagram
    Facebook X (Twitter) Instagram
    SOKALEO
    • HOME
    • KITAIFA
    • KIMATAIFA
    • TETESI ZA SOKA
    • MAGAZETI YA LEO
    • FORUM
    • BOXING
    SOKALEO
    Home » SIMBA SC YAWINDA MAJIBU KWA MLANDAGE, SI KISASI
    KITAIFA

    SIMBA SC YAWINDA MAJIBU KWA MLANDAGE, SI KISASI

    ChikaoBy ChikaoApril 24, 202602 Mins Read
    Share Facebook Twitter Pinterest LinkedIn Tumblr Email
    Share
    WhatsApp Facebook Telegram Twitter Pinterest Email

    BENCHI la ufundi na wachezaji wa Mlandege SC wameweka wazi kuwa wana majibu ya kuwapa wapinzani wao, Simba SC, watakapokutana katika nusu fainali ya Kombe la Muungano. Mchezo huo unatarajiwa kupigwa Jumamosi, Aprili 25, 2026, kwenye Uwanja wa New Amaan Complex, Zanzibar.

    Pambano hilo linatarajiwa kuwa na ushindani mkali kutokana na historia ya timu hizi mbili, huku mshindi akijihakikishia tiketi ya kucheza fainali ya michuano hiyo. Hali hiyo inaongeza presha na hamasa kwa kila upande kuonyesha ubora wao uwanjani.

    Kwa upande wa Simba SC, Meneja wa Idara ya Habari na Mawasiliano, Ahmed Ally, amesema kikosi chao kinaingia kwenye mchezo huo kikiwa na kumbukumbu ya maumivu ya mwaka 2024, walipopoteza ubingwa wa Kombe la Mapinduzi baada ya kufungwa bao 1-0 na Mlandege SC.

    Ameeleza kuwa matokeo hayo bado yapo akilini mwao na yamekuwa chachu ya kuongeza ari kwa wachezaji, wakilenga kufanya vizuri zaidi katika mechi hii muhimu ya nusu fainali.

    Ahmed amesisitiza kuwa Simba haiingii uwanjani kwa lengo la kulipa kisasi, bali kutafuta majibu ya kilichotokea kwenye fainali hiyo na kuthibitisha ubora wao dhidi ya wapinzani hao.

    “Tunawakumbuka walivyotufunga kwenye fainali ya Mapinduzi. Safari hii tunaenda kucheza nao tukiwa na malengo yetu, si kisasi, bali tunataka kujua walitufungaje,” amesema Ahmed.

    Ameongeza kuwa ana imani kubwa na kikosi chao, akisisitiza kuwa ubora waliokuwa nao unawapa nafasi nzuri ya kufikia ndoto ya kutwaa ubingwa wa Kombe la Muungano msimu huu.

    Share. Facebook Twitter Pinterest LinkedIn Tumblr Email
    Previous ArticleSINGIDA BLACK STARS YAREJEA DAR, YAJIPANGA UPYA BAADA YA PIGO MUUNGANO

    Related Posts

    SINGIDA BLACK STARS YAREJEA DAR, YAJIPANGA UPYA BAADA YA PIGO MUUNGANO

    April 24, 2026

    TETESI: YANGA YAHAMISHIA MAJESHI KWA WINGA WA SINGIDA

    April 19, 2026

    KIBABAGE NA KANTE KUUKOSA MCHEZO DHIDI YA NAMUNGO

    April 19, 2026
    Add A Comment
    Leave A Reply Cancel Reply

    LATEST POSTS

    SIMBA SC YAWINDA MAJIBU KWA MLANDAGE, SI KISASI

    SINGIDA BLACK STARS YAREJEA DAR, YAJIPANGA UPYA BAADA YA PIGO MUUNGANO

    TETESI: YANGA YAHAMISHIA MAJESHI KWA WINGA WA SINGIDA

    KIBABAGE NA KANTE KUUKOSA MCHEZO DHIDI YA NAMUNGO

    KAMWE AZUNGUMZA JUU YA YANGA KUMSAJILI “SELEMANI MWALIMU”

    REFA ATUMIA SIMU KAMA VAR

    SINGIDA BLACK STARS WAZIPIGA MKWARA SIMBA, YANGA NA AZAM FC

    © 2026 SOKALEO TANZANIA | All Rights Are Reserved

    Type above and press Enter to search. Press Esc to cancel.