Close Menu
    Facebook X (Twitter) Instagram
    Facebook X (Twitter) Instagram
    SOKALEO
    • HOME
    • KITAIFA
    • KIMATAIFA
    • TETESI ZA SOKA
    • MAGAZETI YA LEO
    • FORUM
    • BOXING
    SOKALEO
    Home » SIMBA YAANZA USAJILI NA MIPANGO YA UWANJA MPYA BUNJU
    KITAIFA

    SIMBA YAANZA USAJILI NA MIPANGO YA UWANJA MPYA BUNJU

    ChikaoBy ChikaoApril 8, 202602 Mins Read
    Share Facebook Twitter Pinterest LinkedIn Tumblr Email
    Share
    WhatsApp Facebook Telegram Twitter Pinterest Email

    KLABU ya Simba tayari imeanza kuandaa mikakati mikubwa kwa ajili ya msimu ujao, ikiwemo usajili wa wachezaji wapya na uwezekano wa kujenga uwanja mpya katika eneo la Bunju.

    Hatua hii imekuja kufuatia mapendekezo ya benchi la ufundi na mazungumzo na mzabuni wa vifaa vya michezo, JayRutty.

    Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi wa Simba, Crescentius Magori, amesema mzabuni huyo hutoa bilioni tano kila mwaka kwa ajili ya ujenzi wa uwanja. Hata hivyo, fedha hizo zinaweza kuangaliwa pia kama zitatumika kuboresha sehemu nyingine za klabu badala ya uwanja wa watu elfu nane.

    “Nimejulishwa na wadhamini wa klabu kwamba mwekezaji ameomba kujenga uwanja kwenye eneo letu la Bunju. Tutakaa naye tuone mipango yake; labda badala ya kutumia bilioni tano kwenye uwanja, tutatumia kuboresha sehemu nyingine,” amesema.

    Magori amefafanua kuwa mabadiliko ya katiba ya klabu yanaendelea kufanyiwa kazi kwa ushirikiano kati ya wadhamini wa klabu na mwekezaji, huku taratibu za kurekebisha mambo kwenye BRELA na sekta nyingine zinazohusiana na uwekezaji huo zikifuatiliwa kwa umakini.

    Kuhusu masuala ya mechi na maamuzi ya waamuzi, Mwenyekiti amewahakikishia mashabiki kuwa viongozi wa klabu hawaruhusiwi kuingilia kati maamuzi hayo.

    “Sisi kama viongozi haturuhusiwi kuingilia kati waamuzi. Haya yametokea kutokana na maamuzi yaliyofanywa kwenye mechi kubwa, tumeiandikia mamlaka na sasa tunasubiri,” amesema.

    Magori amesisitiza umuhimu wa mashabiki kujivunia timu yao na mafanikio yake. “Wanasimba wanapaswa kwanza kujivunia benchi bora na wachezaji bora, mengine yaachwe kwa uongozi,”.

    Kwa upande wa maendeleo ya klabu, amefafanua kuwa msimu huu Simba itatimiza miaka 90 ya uhai wake.

    “Mwaka huu Simba inakwenda kutimiza miaka 90, tutafanya mambo makubwa. Rangi nyekundu ni rangi ya mamlaka; mimi, Mangungu na bodi nzima tuko imara na tayari tumeshaanza usajili wa dirisha kubwa. Hii sio timu ya maneno, kama unataka mpira, njoo Simba,” amesema.

    Kwa hivyo, klabu ya Simba inathibitisha dhamira yake ya kuendeleza miundombinu na kufanya usajili bora, huku ikihakikisha mashabiki wanajivunia timu yao na mafanikio yanayotarajiwa msimu huu.

    Share. Facebook Twitter Pinterest LinkedIn Tumblr Email
    Previous ArticleSURE BOY HATIMAE AOMBA KUSEPA YANGA

    Related Posts

    SURE BOY HATIMAE AOMBA KUSEPA YANGA

    April 8, 2026

    HATIMAE MIGUU IMEANZA KUMSALITI CHAMA

    April 7, 2026

    MPANZU NA FEI TOTO WAKUTANA USO KWA USO KWENYE VITA YA ASSIST

    April 5, 2026
    Add A Comment
    Leave A Reply Cancel Reply

    LATEST POSTS

    SIMBA YAANZA USAJILI NA MIPANGO YA UWANJA MPYA BUNJU

    SURE BOY HATIMAE AOMBA KUSEPA YANGA

    HATIMAE MIGUU IMEANZA KUMSALITI CHAMA

    AFCON EAST AFRICA TAREHE YATANGAZWA

    MPANZU NA FEI TOTO WAKUTANA USO KWA USO KWENYE VITA YA ASSIST

    IBENGE ATANGAZA VITA JUU YA KIKOSI CHA SIMBA

    MBAPPE: NITACHEZEA TIMU YA TAIFA YA CAMEROON

    © 2026 SOKALEO TANZANIA | All Rights Are Reserved

    Type above and press Enter to search. Press Esc to cancel.