Kiungo mzoefu wa klabu ya Yanga, Aboubakar Salum ‘Sure Boy’, ameripotiwa kuomba kuondoka ndani ya kikosi hicho kufuatia kile kinachotajwa kuwa ni kukosa nafasi ya kutosha ya kucheza (playing time).
Sure Boy, ambaye alijiunga na Yanga akitokea Azam FC kufuatia mivutano na waajiri wake wa zamani, anaona ni wakati sahihi wa kutafuta changamoto mpya ambapo atapata nafasi ya kucheza mara kwa mara.
Akiwa na umri wa miaka 36, kiungo huyo fundi anataka kutumia miaka yake ya mwisho uwanjani akiwa anacheza kuliko kusugua benchi.
Ushindani mkubwa wa namba kwenye safu ya kiungo ya Yanga kwa sasa umeonekana kuwa kikwazo kwa nyota huyo, jambo lililompelekea kuomba baraka za uongozi ili aondoke kwa amani.
