Close Menu
    Facebook X (Twitter) Instagram
    Facebook X (Twitter) Instagram
    SOKALEO
    • HOME
    • KITAIFA
    • KIMATAIFA
    • TETESI ZA SOKA
    • MAGAZETI YA LEO
    • FORUM
    • BOXING
    SOKALEO
    Home » NYOTA WATATU WAMTIBULIA LAIZER FOUNTAIN GATE
    KITAIFA

    NYOTA WATATU WAMTIBULIA LAIZER FOUNTAIN GATE

    ChikaoBy ChikaoFebruary 23, 202602 Mins Read
    Share Facebook Twitter Pinterest LinkedIn Tumblr Email
    Share
    WhatsApp Facebook Telegram Twitter Pinterest Email

    KOCHA Mkuu wa Fountain Gate, Mohamed Ismail ‘Laizer’, amesema kuwakosa wachezaji watatu waliofikia makubaliano ya kutua ndani ya kikosi hicho katika dirisha dogo la Januari 2026, ni pigo kubwa kwake, kutokana na matarajio aliyokuwa nayo.

    Nyota walioshindwa kujiunga na timu hiyo katika dirisha dogo ni, mshambuliaji wa Mbeya Kwanza, Boniface Mwanjonde, winga, Tariq Mohamed Mkonga aliyetoka JKU SC ya visiwani Zanzibar na kiungo, Saleh Masoud Abdallah ‘Tumbo’ aliyetokea Pamba Jiji.

    Wachezaji wote watatu, walifikia makubaliano ya kujiunga na timu hiyo na tayari walisaini mikataba ya miaka miwili kwa kila mmoja wao, ingawa dili hizo zilikufa mwishoni, baada ya Fountain Gate kupokea barua rasmi ya kufungiwa kusajili.

    Akizungumza na Soka la Bongo, Laizer, amesema alikuwa na matarajio makubwa kwa wachezaji wote watatu ili wakaongeze nguvu kikosi hicho, lakini dili hizo zilishindikana, jambo lililowavunja moyo benchi lao nzima la ufundi.

    “Kwa sasa tunaendelea kupambana na wachezaji waliopo, kiukweli tulitarajia mambo makubwa kwa sababu ya viwango ambavyo walikuwa navyo katika timu walizotoka, mwenendo wetu sio mzuri, hivyo, tunapaswa kuzidisha juhudi sana,” amesema Laizer.

    Fountain ndio timu ambayo tangu mwaka 2026, umeanza haijaonja ladha ya ushindi katika mechi za Ligi Kuu, tangu mara ya mwisho kikosi hicho kilipoifunga Tanzania Prisons bao 1-0, kwenye Uwanja wa Tanzanite Kwaraa, Babati, Novemba 26, 2025.

    Timu hii iliyohamishia makazi yake kwa sasa jijini Arusha ikiutumia Uwanja wa Sheikh Amri Abeid tangu Nov26 imecheza mechi tano imechapwa tatu na kutoka sare mbili.

    Share. Facebook Twitter Pinterest LinkedIn Tumblr Email
    Previous ArticleSingida Black Stars yaituliza Mtibwa Sugar
    Next Article Mayele Aendelea Kupambana na Ukame wa Mabao Pyramids FC

    Related Posts

    WANA SIMBA WASIFEDHESHWE, TUNAJUA NAMNA YA KUPUNGUZA POINTI

    April 12, 2026

    SIMBA YAANZA USAJILI NA MIPANGO YA UWANJA MPYA BUNJU

    April 8, 2026

    SURE BOY HATIMAE AOMBA KUSEPA YANGA

    April 8, 2026
    Add A Comment
    Leave A Reply Cancel Reply

    LATEST POSTS

    WANA SIMBA WASIFEDHESHWE, TUNAJUA NAMNA YA KUPUNGUZA POINTI

    SIMBA YAANZA USAJILI NA MIPANGO YA UWANJA MPYA BUNJU

    SURE BOY HATIMAE AOMBA KUSEPA YANGA

    HATIMAE MIGUU IMEANZA KUMSALITI CHAMA

    AFCON EAST AFRICA TAREHE YATANGAZWA

    MPANZU NA FEI TOTO WAKUTANA USO KWA USO KWENYE VITA YA ASSIST

    IBENGE ATANGAZA VITA JUU YA KIKOSI CHA SIMBA

    © 2026 SOKALEO TANZANIA | All Rights Are Reserved

    Type above and press Enter to search. Press Esc to cancel.