HomeKITAIFACAF IMEISHA SASA TUNAREJESHA HESHIMA LIGI KUU

CAF IMEISHA SASA TUNAREJESHA HESHIMA LIGI KUU

BAADA kuondolewa  katika michuano ya Ligi ya Mabingwa Afrika, Kocha Mkuu wa Simba SC, Steve Barker, ameweka wazi malengo yake mapya akiwataka wachezaji wake kuhamishia nguvu zote kwenye mashindano ya Ligi Kuu Tanzania Bara.

Barker aliyasema hayo mara baada ya kumalizika kwa dakika 90 za mchezo wa mwisho wa hatua ya makundi ya Ligi ya Mabingwa Afrika dhidi ya Stade Malien, ambapo Simba iliibuka na ushindi wa bao 1-0 katika Uwanja wa Benjamin Mkapa  jijini Dar es Salaam.

Licha ya ushindi huo, matokeo ya jumla hayakutosha kuiwezesha Simba kusonga mbele, jambo lililowafanya kuaga rasmi mashindano hayo.

Barker amesema amefurahishwa na kiwango kilichoonyeshwa na wachezaji wake, akisisitiza kuwa ameona mabadiliko chanya na ukuaji mkubwa wa kikosi chake kadri mashindano yalivyokuwa yakiendelea.

Kocha huyo ameeleza  kuwa sasa ni wakati wa kuangalia mbele na kujipanga upya kwa ajili ya malengo yaliyosalia ndani ya msimu huu, kuwa Ligi Kuu Tanzania Bara ni fursa muhimu kwa timu hiyo kurejesha heshima na kuonyesha ubora wao.

“Tumeondolewa kwenye mashindano ya Ligi ya Mabingwa Afrika, lakini bado tuna Ligi Kuu Tanzania Bara. Tunakwenda kujiandaa vizuri na kupambana kutafuta matokeo chanya katika kila mechi,” amesema Barker.

Ameongeza  kuwa dhamira yao ni kuhakikisha wanamaliza msimu wakiwa katika nafasi nzuri itakayowapa nafasi ya kushiriki tena Ligi ya Mabingwa Afrika msimu ujao, akiamini kuwa uzoefu walioupata msimu huu utakuwa chachu ya mafanikio yajayo.

RELATED ARTICLES

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Most Popular