Yanga Yaagana Rasmi na Kocha Manqoba Mngithi

Uongozi wa klabu ya Young Africans Sports Club umetoa taarifa rasmi kwa umma leo Oktoba 24, 2026, ukitangaza kufikia uamuzi mzito wa kuvunja mkataba na Kocha Mkuu wa timu hiyo ya kwanza, Manqoba Mngqithi.
Katika taarifa hiyo iliyotolewa na Afisa Mtendaji Mkuu wa klabu, imeelezwa kuwa uongozi pia umesitisha mkataba na Kocha wa Viungo wa timu hiyo, Chyna Mokaila, huku ukiwashukuru watendaji hao kwa mchango wao na kuwatakia kila la kheri kwenye majukumu yao mapya.
Uamuzi huu uja kufuatia mwenendo wa hivi karibuni wa timu hiyo kwenye Ligi Kuu ya NBC, ambapo uongozi umethibitisha kuwa tayari mchakato wa haraka wa kumpata Kocha Mkuu mpya umeanza na unatarajia kukamilika hivi karibuni.






