Ruka hadi maudhui
SOKALEO

Huyu Hapa Mchezaji Wa Kenya Anaetamba La Liga ni Balaa

Chikao
Huyu Hapa Mchezaji Wa Kenya Anaetamba La Liga ni Balaa
Mshambuliaji wa kimataifa wa Kenya, Job Ochieng, ameendelea kuweka viwango vya juu barani Ulaya baada ya kuhusika moja kwa moja katika mabao yote matatu kwenye ushindi wa mabao 3-2 iliyopata Real Sociedad dhidi ya Elche katika muendelezo wa Ligi Kuu nchini Hispania (La Liga).
​Ochieng alianzia kwenye kikosi cha kwanza na kufungua ukurasa wa mabao katika dakika ya 11, kabla ya kuonyesha ufundi wake kwa kutoa pasi mbili za mabao (assists) katika dakika ya 32 na dakika ya 90 ya mchezo huo. Kiwango hicho cha kuvutia kimekuja kama muendelezo wa mabadiliko makubwa aliyoanza kuyaonyesha tangu mchezo wake dhidi ya miamba Real Madrid.
​Kipaji hiki kutoka Afrika Mashariki kinazidi kujithibitisha katika ngazi ya juu zaidi ya soka la kimataifa, ikitoa matumaini makubwa kwa timu ya taifa ya Kenya (Harambee Stars) kuelekea maandalizi ya michuano ya Kombe la Mataifa ya Afrika (AFCON).
Shiriki:

Habari Zinazohusiana

Zaidi →