HISPANIA INAWEZA KUIFUNGA UFARANSA NA KUITOA

Arsène Wenger amezua mjadala mkubwa baada ya kudai kuwa Ufaransa ndiyo timu itakayobeba Kombe la Dunia 2026, huku akisisitiza kuwa kasi ya mchezo wa kisasa ndiyo inayobeba mafanikio.
Mkurugenzi wa Maendeleo ya Soka wa FIFA, Arsène Wenger, amesema anaelewa baadhi ya watu wanaweza kudhani anaipa upendeleo Ufaransa, lakini kwa mtazamo wake Les Bleus ndiyo timu yenye nafasi kubwa ya kutwaa Kombe la Dunia 2026.
Wenger ameeleza kuwa mashindano ya mwaka huu yanachezwa kwa kasi kubwa sana, hivyo timu zinazoshindwa kuendana na kasi hiyo pamoja na ubora wa kiufundi haziwezi kufika mbali.
Aidha, amesema timu nyingi za Asia ziliondolewa mapema kwa sababu zilishindwa kuhimili kiwango hicho cha mchezo. Pia ameitaja Hispania kuwa ndiyo timu yenye uwezo mkubwa wa kuizuia Ufaransa ikiwa itafuzu hatua inayofuata.






