Home KITAIFA MAJERUHI YAWALAZIMISHA PEDRO KUBADILI KIKOSI YANGA

MAJERUHI YAWALAZIMISHA PEDRO KUBADILI KIKOSI YANGA

0
84

KOCHA Mkuu wa Yanga, Pedro Goncalves ameweka wazi kuwa kutakuwa na mabadiliko katika kikosi cha timu hiyo kitakachoshuka dimbani kuvaana na Polisi Tanzania kwenye mchezo wa hatua ya 32 bora wa Kombe la Shirikisho la CRDB.

Mabadiliko hayo yanatarajiwa kuonekana katika kikosi cha kwanza kitakachoanza mchezo huo muhimu wa mtoano.

Mabingwa hao watetezi wanatarajiwa kushuka katika dimba la KMC Complex, Mwenge jijini Dar es Salaam, wakimenyana na Polisi Tanzania ambao wanashiriki Ligi ya Championship, saa 1:15 usiku.

Mchezo huo  unatarajiwa kuwa na ushindani mkubwa huku kila timu ikipania kusonga mbele katika hatua inayofuata ya mashindano hayo.

Akizungumza kuelekea mchezo huo, Goncalves amesema wanaiheshimu Polisi Tanzania licha ya kucheza ligi ya daraja la chini. Ameeleza kuwa katika mashindano ya mtoano kila timu huwa na nafasi ya kufanya vizuri, hivyo wamejipanga kuhakikisha wanapata ushindi.

Kocha huyo amesema baadhi ya mabadiliko kwenye kikosi chake yamelazimishwa na hali ya majeruhi waliyonayo baadhi ya wachezaji. Kutokana na hali hiyo, benchi la ufundi linalazimika kuwapa nafasi wachezaji wengine ili kuendelea kuimarisha timu.

Ameongeza kuwa licha ya changamoto hiyo, ana imani wachezaji watakaopewa nafasi wataonyesha uwezo mkubwa uwanjani na kupambana kwa nguvu ili kuhakikisha wanapata matokeo chanya dhidi ya Polisi Tanzania.

“Kukosekana kwa baadhi ya wachezaji kunatulazimisha kufanya mabadiliko, lakini tuna matumaini wale watakaopata nafasi watapambana kwa nguvu ili kupata ushindi na kusonga mbele katika mashindano haya,” amesema Goncalves.

Kocha huyo pia amewashukuru mashabiki wa Yanga kwa sapoti kubwa waliyoonyesha katika mchezo uliopita dhidi ya Singida Black Stars, amesema  anaamini wataendelea kuisapoti timu katika michezo ijayo kwani mchango wao unaifanya timu kuwa na nguvu zaidi kama mchezaji wa 12 uwanjani.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here