HomeKITAIFADEPU VUA KINYAGO WEWE NI BALOTELI

DEPU VUA KINYAGO WEWE NI BALOTELI

Mshambuliaji wa kimataifa kutoka Angola, Depu, anaendelea kuthibitisha ubora wake ndani ya kikosi cha Young Africans SC kwa kuwa tegemeo muhimu la mabao tangu alipojiunga na klabu hiyo ya Jangwani.

Katika michezo sita aliyocheza hivi karibuni, Depu amehusika moja kwa moja kwenye mabao sita akifunga mabao matano na kutoa pasi moja ya bao takwimu zinazoonyesha ufanisi wake mkubwa katika safu ya ushambuliaji.

Ameonyesha makali zaidi katika michezo dhidi ya Kabylie na Dodoma Jiji, akifunga mabao mawili kila timu, huku akiongeza bao moja dhidi ya Mashujaa. Hata hivyo, hakufanikiwa kufunga katika michezo miwili dhidi ya Al Ahly pamoja na mchezo mmoja dhidi ya AS FAR.

Kwa mwenendo huu, Depu anaendelea kuwa moja ya silaha kuu ya ushambuliaji kwa Yanga katika mashindano ya ndani na kimataifa.

RELATED ARTICLES

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Most Popular