Shirikisho la Soka Barani Afrika (CAF) limetangaza rasmi kuwa Tuzo za CAF 2025 zitafanyika mjini Rabat, Morocco siku ya Jumatano, Novemba 19, 2025.
Kwa mujibu wa taarifa ya CAF, hafla hiyo ya kifahari itaanza saa 1 jioni kwa saa za Morocco (saa 3 usiku kwa saa za Cairo), katika ukumbi ambao bado haujatajwa.
Tuzo hizo ni mojawapo ya matukio makubwa zaidi katika kalenda ya soka la Afrika, zikilenga kutambua na kuheshimu wanamichezo bora wa bara katika vipengele mbalimbali.
Miongoni mwa tuzo zitakazotolewa ni:
🏆 Mchezaji Bora wa Afrika (Wanaume na Wanawake)
🎯 Kocha Bora wa CAF (Wanaume na Wanawake)
🌍 Timu Bora ya Taifa ya Mwaka (Wanaume na Wanawake)
⚽ Klabu Bora ya Mwaka (Wanaume na Wanawake)
🌟 Mchezaji Bora Chipukizi wa CAF
Tuzo hizi za kila mwaka huchochea hamasa na ushindani miongoni mwa wachezaji na makocha, huku zikionyesha maendeleo ya mchezo wa soka barani Afrika.










Leave a Reply