Kocha Mgunda Akiri Kua Wanaenda Kucheza na Timu Ngumu

Kuelekea mchezo wao mkubwa wa Ligi Kuu dhidi ya Simba SC, Kocha Mkuu wa Namungo FC, Juma Mgunda, ameweka wazi kuwa kikosi chake kimefanya maandalizi ya kutosha na kiko tayari kwa ajili ya mtanange huo. Akizungumza na waandishi wa habari, Mgunda alisisitiza kuwa kuwakabili Simba siyo suala la kuogopa, bali ni utekelezaji wa kanuni za soka la ushindani za kumheshimu mpinzani wao ambaye anaongoza msimamo wa ligi na ana kikosi bora chenye wachezaji wazuri.
Akizungumzia rekodi za nyuma, kocha huyo alikiri wazi changamoto wanazokutana nazo dhidi ya wekundu hao wa Msimbazi, akisema: "Ukweli ni kwamba ni kweli toka nimekwenda Namungo hatujawai kupata matokeo mazuri Hilo liko wazi na tunaelewa hivyo tunafahamu hivyo na ndio maana nimekuambia kwamba kesho tunacheza na timu nzuri yenye wachezaji wazuri." Hata hivyo, alieleza kuwa hali hiyo imewafanya wajipange upya kufanyia kazi mapungufu yao ili kupata matokeo chanya.
Aidha, Mgunda alithibitisha kuwa kikosi chako kiko katika hali nzuri isipokuwa mchezaji Gamba Matiko pekee ambaye atakosekana kwenye mchezo huo kutokana na kusumbuliwa na jeraha dogo la kifundo cha mguu (ankle) kwa ushauri wa madaktari. Alihitimisha kwa kueleza kuwa kucheza kwenye uwanja wenye nyasi bandia hakutakuwa na changamoto kubwa kwa upande wao, huku akisisitiza kuwa wanatazamia kuona mchezo wenye ushindani mkubwa wa dakika 90.






