Farhan Aumia Sana Kocha Fadlu Kwenda Yanga

Shabiki wa Simba SC, Farham Kihamu, ametoa ujumbe wa hisia kwa kocha Fadlu Davids kufuatia kujiunga kwake na Young Africans (Yanga), akieleza kuwa licha ya kuumia kumuona akiwa kwenye jezi ya kijani na njano, anaelewa kuwa soka ni sehemu ya ajira kwa makocha na wachezaji.
Kupitia ukurasa wake wa Instagram, Farham amesema kuwa mpira wa miguu ni mchezo wenye hisia kali kwa mashabiki na wanachama, lakini kwa makocha na wachezaji ni ajira inayowawezesha kutimiza majukumu yao ya maisha na familia.
Katika ujumbe wake, Farham amemsifu Davids kwa kumwelezea kuwa ni kocha bora, akisisitiza kuwa hatabadilisha mtazamo wake kuhusu uwezo wake kwa sababu tu sasa anaitumikia Yanga, ambayo ni mpinzani wa Simba.
Pia amemtakia kila la heri katika ukurasa mpya wa maisha yake, akieleza kuwa anaamini uwezo, ubinadamu na utu wa kocha huyo. Amehitimisha ujumbe wake kwa maneno: “Ikawe kheri sana and all the best Gaffer Fadlu Davids.”






