Mikel Arteta Kuongeza Mkataba wa Kusalia Arsenal.

Kocha wa Arsenal, Mikel Arteta, amefikia makubaliano ya awali ya mkataba mpya wa muda mrefu wa kuendelea kuinoa klabu hiyo.
Kwa mujibu wa taarifa hizo, makubaliano hayo yanajumuisha ongezeko la mshahara kwa Arteta, kufuatia kazi nzuri aliyoifanya katika misimu ya hivi karibuni.
Arteta anatajwa kuwa sehemu muhimu ya mpango wa muda mrefu wa Arsenal, huku klabu hiyo ikiendelea kujenga kikosi chenye ushindani wa juu.
Ingawa mkataba huo bado haujasainiwa rasmi, pande hizo tayari zimefikia makubaliano ya mdomo, na saini ya Arteta inatarajiwa kukamilishwa hivi karibuni.
Taarifa hiyo pia imeripotiwa na BBC, huku vyanzo vilivyo karibu na kocha huyo vikithibitisha kuwa makubaliano yamefikiwa.






