Ruka hadi maudhui
SOKALEO

Kwa Mara ya Kwanza Tangu 2007 Ronaldo Akosa Tuzo Ureno.

Chikao
Kwa Mara ya Kwanza Tangu 2007 Ronaldo Akosa Tuzo Ureno.

Nyota wa soka wa Ureno Cristiano Ronaldo hakupokea tuzo yoyote binafsi wala tuzo maalum katika Sherehe za Tuzo za Shirikisho la Soka la Ureno (FPF) za mwaka 2026.

Hali hiyo imekuwa ikitajwa kuwa jambo lisilo la kawaida kwa Ronaldo, ambaye kwa takribani miongo miwili tangu mwaka 2007 mpaka 2025 amekuwa akipokea tuzo mbalimbali za binafsi nchini Ureno.

Kwa sehemu kubwa ya maisha yake ya soka, Ronaldo amekuwa akitwaa tuzo ya Mchezaji Bora wa Mwaka wa Ureno huku katika miaka ambayo hakushinda tuzo hiyo akitunukiwa tuzo maalum zikiwemo tuzo ya Mafanikio ya Maisha (Lifetime Achievement Award).

Hata hivyo, katika hafla ya mwaka huu Ronaldo alihudhuria bila kuondoka na tuzo yoyote.

Shiriki:

Habari Zinazohusiana

Zaidi →

Vigogo wa Ulaya Kukipiga Leo Kwenye UEFA

Dani Carvajal aondoka Madrid baada ya miaka 23

MICHAEL OWEN: Ni mapema mno kumfukuza Carrick Manchester United

Kunyoa kumenipa faragha mtaani, watu hawanitambui – Haaland