Ruka hadi maudhui
SOKALEO

Kocha wa Kenya Afichua Kushindwa Kuishi Kenya Kisa Kukosa Kibali.

Chikao
Kocha wa Kenya Afichua Kushindwa Kuishi Kenya Kisa Kukosa Kibali.

Kocha mkuu wa timu ya taifa ya Kenya Harambee Stars Benni McCarthy, amefichua sababu inayomfanya kuondoka nchini humo kila baada ya kumalizika kwa kambi ya timu.

McCarthy amesema yeye pamoja na baadhi ya wataalamu wa kigeni katika benchi lake la ufundi wamekuwa nchini Kenya kwa takribani miezi 18 bila kupata vibali vya kufanya kazi.

Kocha huyo amesema hali hiyo inamlazimisha kuingia nchini kwa ajili ya kazi wakati wa kambi na kuondoka mara tu kambi inapomalizika.

“Hatuwezi kufanya kazi kama wahamiaji wasio halali. Nakuja, nafanya kazi yangu, kisha naondoka kambi inapomalizika,” alisema McCarthy.

Mbali na suala la vibali vya kazi, McCarthy pia ameeleza wasiwasi kuhusu malipo ya posho za wachezaji wa Harambee Stars.

Kwa mujibu wa kocha huyo, baadhi ya wachezaji wamehudhuria kambi nne hadi tano bila kupokea posho walizoahidiwa.

“Kutopokea hata senti moja ya kile ulichoahidiwa utaanza kujiuliza, je, inafaa? Je, hivi ndivyo inavyopaswa kuwa kwa timu ya taifa?” amesema McCarthy.

Shiriki:

Habari Zinazohusiana

Zaidi →

Vigogo wa Ulaya Kukipiga Leo Kwenye UEFA

Dani Carvajal aondoka Madrid baada ya miaka 23

MICHAEL OWEN: Ni mapema mno kumfukuza Carrick Manchester United

Kunyoa kumenipa faragha mtaani, watu hawanitambui – Haaland