Ruka hadi maudhui
SOKALEO

WALITAKA KUMUUA MESSI KWA BOMU KWENYE KOMBE LA DUNIA

Chikao
WALITAKA KUMUUA MESSI KWA BOMU KWENYE KOMBE LA DUNIA

Ripoti za siri za jeshi la polisi nchini Marekani zimefichua kuwepo kwa vitisho vikubwa vya kuuawa kwa mlipuko vilivyomlenga nahodha wa Argentina, Lionel Messi, wakati wa michuano ya hivi karibuni ya Kombe la Dunia la FIFA 2026.

Nyaraka hizo zilizovuja kutoka kwa shirika la upelelezi la FBI na Kituo cha Kimataifa cha Ushirikiano wa Polisi (IPCC), zinasema Messi ndiye aliyekuwa mchezaji aliyetishiwa zaidi maisha kuliko nyota wengine wote kwenye michuano hiyo.

Tishio la kwanza lilikuwa kwenye mchezo wa Argentina dhidi ya Jordan, ambapo kabla ya mchezo huo mwanamume mmoja alipiga simu kwenye uwanja wa ndege wa Dallas na kutishia kuwa yeye na wenzake wawili walikuwa wanaelekea uwanjani wakiwa na mabomu ya kutengeneza nyumbani na bunduki aina ya AR-15. Alimtaja Messi kama mlengwa wao mkuu.

Tishio lingine lilikuwa dhidi ya mechi na Egypt, ambapo kabla ya mchezo huo wa hatua ya 16 bora, mtumiaji mmoja wa mtandao wa X alichapisha ujumbe akitishia kuingia kwenye uwanja wa Atlanta akiwa amejifunga mabomu manne mwilini mwake ili kumlipua Messi.

Polisi walipokea onyo lingine kuwa kulikuwa na mabomu yametegwa ndani ya mapipa ya takataka ya uwanja huo, hali iliyolazimu vikosi vya usalama na mbwa maalum kukagua uwanja mzima.

Shiriki:

Habari Zinazohusiana

Zaidi →

Vigogo wa Ulaya Kukipiga Leo Kwenye UEFA

Dani Carvajal aondoka Madrid baada ya miaka 23

MICHAEL OWEN: Ni mapema mno kumfukuza Carrick Manchester United

Kunyoa kumenipa faragha mtaani, watu hawanitambui – Haaland