SUZUKI WA JAPAN KIPA MPYA PSG

Klabu imefikia makubaliano ya kumsajili kipa wa timu ya Taifa ya Japan Zion Suzuki kuwa kipa wao mpya akitokea Parma ya Italia.
Kwa mujibu wa Fabrizio Romano, Makubaliano kati ya klabu hizo mbili yamekamilika kwa thamani ya jumla ya Euro milioni 35 kama ilivyofichuliwa hivi karibuni; Suzuki atasaini mkataba wa muda mrefu na Paris.
Sasa Suzuki anaweza kuondoka Paris kwa mkopo ili kupata nafasi zaidi ya kucheza, huku Juventus ikiwa na uwezekano wa kumsajili hivi karibuni.






