Mchawi wa mpira na gwiji wa soka nchini Brazil, Ronaldinho Gaucho, ametangaza kurejea uwanjani baada ya miaka 11 tangu alipoweka kandanda pembeni!
Ronaldinho (46) anaripotiwa kusaini mkataba rasmi na klabu ya Ravenna FC inayoshiriki Ligi Daraja la Tatu nchini Italia (Serie C). Dhumuni kuu la kurejea kwa mshindi huyo wa Ballon d’Or ni kufunga goli la mwisho la taaluma yake (final goal) na kutoa zawadi ya kipekee ya burudani kwa mashabiki wa klabu hiyo na jiji la Ravenna.
Je, unaamini uchawi wa miguu wa Ronaldinho bado uko pale pale hata akiwa na miaka 46? Dondosha maoni yako!