LUKAKU ATIMKIA LIGI KUU YA UTURUKI

Klabu ya FENERBAHCE imeripotiwa kufikia makubaliano ya kumsaini mshambuliaji raia wa Ubelgiji Romelo Lukaku.
Kwa mujibu wa Fabrizio Romano, Makubaliano ya mdomo yamefikiwa na Napoli kwa ada ya zaidi ya Euro milioni 6, huku nyaraka na taratibu za kimaandishi zikipitiwa leo ili kukamilisha dili hilo.
Lukaku tayari amekubaliana na masharti binafsi na anatarajiwa kusafiri hadi Istanbul mara tu klabu itakapotoa idhini ya mwisho.






