Klabu ya Barcelona imefikia makubaliano ya mdomo na kipa wa Kimataifa wa Croatia, Dominik Livaković, anayekipiga kupitia klabu ya Fenerbahçe ya nchini Uturuki, ili kujiunga na miamba hiyo ya Hispania. Taarifa kutoka kwa mwandishi mahiri wa habari za michezo, Carlos Monfort, zinathibitisha kuwa pande zote zimefikiana muafaka mzuri huku dili hili likitarajiwa kukamilika rasmi kwa dau la awali la Euro milioni 2 pamoja na bonasi ya Euro milioni 2 za ziada.
Mpango uliopo wa Barcelona kwa kipa huyo mwenye uzoefu ni kumsajili na kisha kumtoa kwa mkopo kwa msimu huu kabla ya kurejea rasmi kikosini kuanzia Juni 2027. Hatua hii inalenga kujiimarisha kwa siku za usoni huku klabu ikijipanga na maisha baada ya kipa Wojciech Szczęsny ambaye mkataba wake unatarajiwa kufika ukingoni na kuondoka klabuni hapo.
Ujio wa Livaković unatajwa kuwa ni moja ya mikakati thabiti ya viongozi wa Barcelona katika kuhakikisha safu yao ya makipa inakuwa na wachezaji wa akiba wenye uwezo mkubwa wa kupambana kwenye michuano yote mikubwa msimu ujao na miaka ijayo bila kupoteza ubora uwanjani.