Ruka hadi maudhui
SOKALEO

WACHEZAJI WA REAL MADRID WAPIGANA KISA MBAPPE

Chikao
WACHEZAJI WA REAL MADRID WAPIGANA KISA MBAPPE

Kiungo wa klabu ya Real Madrid, Federico Valverde na mwenzake Aurélien Tchouaméni wanadaiwa kuingia kwenye ugomvi mkubwa wakati wa mazoezi ya timu hiyo, huku mvutano wao ukielezwa kuendelea hadi ndani ya chumba cha kubadilishia nguo.

Kwa mujibu wa taarifa mbalimbali zinazozunguka kwenye vyombo vya habari vya michezo barani Ulaya, wawili hao walionekana kutofautiana vikali jambo lililosababisha hali ya sintofahamu ndani ya kikosi hicho cha mabingwa wa Hispania. Tukio hilo limezua maswali mengi kuhusu hali ya umoja na mshikamano ndani ya timu hiyo kuelekea mechi muhimu za msimu.

Ripoti hizo pia zinaeleza kuwa hali ya mahusiano ndani ya kikosi cha Real Madrid imeendelea kuwa ya wasiwasi katika siku za hivi karibuni, huku baadhi ya wachezaji wakidaiwa kutoridhishwa na mwenendo wa mambo ndani ya timu.

Tukio hilo linatajwa kuja wakati sakata linalomhusu nyota wa klabu hiyo, Kylian Mbappé, bado linaendelea kuzua mjadala mkubwa miongoni mwa mashabiki na wachambuzi wa soka, jambo linaloonyesha wazi kuwepo kwa changamoto za ndani ndani ya miamba hiyo ya soka Ulaya.

Shiriki:

Habari Zinazohusiana

Zaidi →

Vigogo wa Ulaya Kukipiga Leo Kwenye UEFA

Dani Carvajal aondoka Madrid baada ya miaka 23

MICHAEL OWEN: Ni mapema mno kumfukuza Carrick Manchester United

Kunyoa kumenipa faragha mtaani, watu hawanitambui – Haaland