Atletico au Barca, nani atakaa kileleni La Liga

Leo usiku, viwanja vya Riyadh Air Metropolitano vitasimama kwa dakika 90 nzuri za mchezo wa mzunguko wa 12 wa Ligi Kuu ya Hispania (La Liga), pale wenyeji Atlético Madrid watakapowakaribisha wababe FC Barcelona katika pambano linalobeba taswira ya ubingwa mapema.
Kwa sasa, Barcelona inaongoza msimamo wa ligi ikiwa na alama 30, ikifuatiwa kwa karibu sana na Atlético Madrid wenye alama 28. Ushindi kwa vijana wa Diego Simeone utawawezesha kupindua meza na kukaa kileleni mwa msimamo, wakati Hansi Flick na kikosi chake cha Barcelona wakisaka ushindi ili kutanua goli hadi kufikia alama tano mbele






