Ruka hadi maudhui
SOKALEO

TANZIA: Shabiki Maarufu wa Yanga, Mzee Mpili, Afariki Dunia

Chikao
TANZIA: Shabiki Maarufu wa Yanga, Mzee Mpili, Afariki Dunia

Shabiki maarufu wa klabu ya Yanga, Mzee Mpili, amefariki dunia usiku wa kuamkia leo katika eneo la Ikwiriri, Wilaya ya Rufiji.

Kwa mujibu wa taarifa zilizotolewa, Mzee Mpili alikuwa akisumbuliwa na changamoto mbalimbali za kiafya, ikiwemo matatizo ya mgongo na kiuno, pamoja na maradhi yanayohusiana na umri.

Mzee Mpili alikuwa akifahamika miongoni mwa mashabiki wa Yanga kutokana na upendo wake mkubwa kwa klabu hiyo na mara kwa mara alionekana akiiunga mkono timu yake.

Kifo chake kimepokelewa kwa huzuni na majonzi na familia, ndugu, jamaa, marafiki pamoja na mashabiki wa Yanga.

Mungu ailaze roho ya marehemu Mzee Mpili mahali pema peponi. Pole kwa familia, ndugu, jamaa, marafiki na familia nzima ya wana-Yanga kwa msiba huu.

Shiriki:

Habari Zinazohusiana

Zaidi →

Kocha wa Simba Steve Barker Awasha Moto Mpya

YAMAL: Afikisha mchango wa mabao 20 ndani ya mechi 13