Mbappe anaamini ana nafasi ya kushinda Ballon D’Or.

Mshambuliaji wa Real Madrid Kylian Mbappé ameonyesha wazi kuwa anaamini ana nafasi ya kushinda tuzo ya Ballon d’Or, huku akitaja mafanikio yake makubwa msimu huu.
Akizungumza na waandishi wa habari, nyota huyo alisema:
“Nimeandika historia msimu huu katika mashindano yenye hadhi kubwa zaidi, lakini bado kuna safari ndefu. Huenda huu ukawa mwaka mzuri kwa Ballon d’Or, lakini waandishi wa habari ndio hupiga kura na wao ndio wataamua.”
Mbappé hata hivyo amesema hataki kujipa presha kubwa kuhusu tuzo hiyo, akisisitiza kuwa jambo muhimu kwake ni kuendelea kufanya vizuri uwanjani.
“Mimi naangalia tu kufanya kila ninachoweza.”
Je, Mbappé anastahili Ballon d’Or msimu huu?






