Kiungo wa Yanga SC, Duke Abuya, amepata wito wa kujiunga na timu ya taifa ya Kenya (Harambee Stars) kuelekea mechi za kufuzu Ligi ya Mataifa ya Afrika (AFCON) 2027 dhidi ya Eritrea na Guinea.
Mchezaji huyo anayeonyesha kiwango bora hivi sasa anatarajiwa kuwa msaada mkubwa na kuongeza nguvu katika safu ya kiungo wakati Harambee Stars ikianza kampeni yake ya kusaka nafasi ya kushiriki michuano hiyo ya barani Afrika.