Hii Hapa Mipango ya Yanga Kuelekea Kariakoo Dadi October 10

UONGOZI wa Yanga SC umeweka wazi kuwa kutakuwa na muda wa mapumziko kwa wachezaji wa timu hiyo kwa muda wa siku 8 huku wakiendelea na program za mazoezi.
Timu hiyo mchezo wake wa mwisho ulikuwa wa kirafiki dhidi ya St George ikipata ushindi wa bao 1-0 likifungwa na Albert Kangwanda Uwanja wa Uhuru.
Kamwe ameweka wazi kuwa mara baada ya mchezo huo wapo wachezaji ambao watakwenda kwenye majukumu ya taifa na wengine watabaki kambini wataendelea na program pamoja na mapumziko kabla ya kurejea kambini.
“Mpango uliopo kwa sasa kuna wachezaji ambao wanakwenda kwenye majukumu ya taifa na kutakuwa na mapumziko ya siku 8 wachezaji watapewa na kutakuwa na program ya mazoezi kwa wachezaji ambao hawatakuwa kwenye majukumu kwenye timu za taifa,”.
Mchezo ujao kwa Yanga SC kwenye ligi unatarajiwa kuchezwa Oktoba 10, 2026 itakuwa dhidi ya Simba SC Kariakoo Dabi ya mzunguko wa kwanza msimu wa 2026/27.






