SIMBA SC IPO MBINONI KUSHUSHA MSHAMBULIAJI HUYU HAPA MPYA

Klabu ya Simba SC ipo kwenye hatua za mwisho kabisa za kukamilisha usajili wa mshambuliaji wa JKT Tanzania, Paul Peter Kasunda (27), ili kuimarisha safu yao ya ushambuliaji kuelekea msimu mpya wa mashindano.
Tayari mchezaji huyo amekubaliana masharti yote binafsi na Wekundu wa Msimbazi, na hivi sasa uongozi wa Simba upo kwenye hatua za mwisho kumalizana na klabu yake ya JKT Tanzania kabla ya kumtambulisha rasmi kwa mashabiki.
Hatua ya Simba kumgeukia Kasunda imekuja mara baada ya ofa yao waliyoiwasilisha kwa klabu ya Al-Tahaddy ya Libya ili kumnasa winga raia wa Senegal, Pape Abdou N’diaye, kupigwa chini. Kufuatia kukwama kwa dili hilo la N’diaye, viongozi wa Simba wameamua kuingia sokoni kwa haraka na kumfuata Kasunda ili kuziba pengo hilo na kuongeza nguvu kwenye eneo la mbele.
Hivi sasa usajili huo wa Paul Peter Kasunda kuelekea Msimbazi unatajwa kuwa karibu kukamilika kwa asilimia kubwa na muda wowote atatambulishwa. Unauonaje uamuzi huu wa Simba kumleta Kasunda kikosini badala ya N’diaye? Dondosha maoni yako!






