Ruka hadi maudhui
SOKALEO

SHALULILE ASEMA TUKIWA PAMOJA TUTASHINDA MAKOMBE

Chikao
SHALULILE ASEMA TUKIWA PAMOJA TUTASHINDA MAKOMBE
Mshambuliaji mpya wa Yanga SC, Peter Shalulile, amesema umoja kati ya wachezaji, viongozi na mashabiki ni jambo muhimu katika safari ya klabu hiyo ya kusaka mafanikio msimu mpya.Akizungumza na waandishi wa habari wakati wa utambulisho wake rasmi Agosti 3, 2026, katika makao makuu ya Yanga yaliyopo Jangwani, Shalulile amesema kila upande ndani ya klabu unapaswa kuwa na mshikamano ili kufikia malengo yaliyowekwa.
Kwa mujibu wa Shalulile, nguvu ya Yanga haitatokana na wachezaji pekee, bali pia ushirikiano kutoka kwa viongozi na sapoti ya mashabiki katika kila hatua ya msimu.Lengo kubwa ni moja kupambana kwa pamoja na kuhakikisha Yanga inatwaa makombe.
Mbali na hilo, Shalulile amezungumzia hamu yake ya kucheza Kariakoo Derby dhidi ya Simba SC, akisema amesikia kuwa mchezo huo ni miongoni mwa matukio makubwa na ya kuvutia zaidi katika soka la Tanzania.Mshambuliaji huyo wa Namibia amesema anatamani kuipitia mwenyewe hali ya uwanja, presha na hisia zinazozunguka mchezo kati ya vigogo hao wa soka la Tanzania.
Shiriki:

Habari Zinazohusiana

Zaidi →

Kocha wa Simba Steve Barker Awasha Moto Mpya

YAMAL: Afikisha mchango wa mabao 20 ndani ya mechi 13