Rasmi, Jonas Mkude, aliyewahi kuitumikia Simba SC na Yanga SC, amejiunga na Mashujaa FC ya Kigoma kuelekea msimu mpya wa mashindano.Jonas Mkude ameanza ukurasa mpya wa maisha yake ya soka baada ya kujiunga rasmi na Mashujaa FC, akielekea kuwa sehemu ya kikosi kitakachoshiriki NBC Premier League pamoja na CRDB Federation Cup msimu wa 2026/27.
Mkude anaingia Mashujaa akiwa na uzoefu mkubwa wa soka la Tanzania, baada ya kujenga historia ndani ya vilabu vikubwa vya Kariakoo, Simba SC na Yanga SC.Ujio wake unatarajiwa kuongeza uzoefu, utulivu na ushindani katika eneo la kiungo ndani ya kikosi cha Mashujaa. Karibu Kigoma, Jonas Mkude! Kiungo mwenye historia kubwa sasa anaingia kwenye himaya ya Watanganyika.