Ruka hadi maudhui
SOKALEO

Kamwe: Hii Yanga ni Ya Asilimia 25% tu, Bado Hatujaonyesha Zote

Chikao
Kamwe: Hii Yanga ni Ya Asilimia 25% tu, Bado Hatujaonyesha Zote
Afisa Habari na Mawasiliano wa Yanga SC, Ally Kamwe, ametoa kauli nzito kuhusu kiwango cha timu hiyo kwasasa kufuatia mwanzo wao wa Ligi Kuu ya NBC ambapo wamefanikiwa kufunga jumla ya mabao 7 katika michezo miwili ya kwanza.
​Akizungumza mara baada ya mchezo wao, Kamwe amewataka mashabiki na wapinzani kutofikiri kuwa Yanga ipo kwenye kilele cha ubora wake. Amebainisha kuwa mchezo na spidi inayoonekana hivi sasa ni kama asilimia 25 (25%) tu ya kile ambacho kocha anakitengeneza kwenye uwanja wa mazoezi, na kwamba baada ya mwezi mmoja timu hiyo itakuwa kwenye kiwango cha hatari zaidi.
​Kuhusu mjadala wa timu hiyo kuruhusu magoli katika michezo ya hivi karibuni badala ya kutoka na hati safi (clean sheet), Kamwe amejibu kwa msisitizo:
​”Shida yenu nyie Yanga inaposhinda mnatafuta ajenda ya kujadili. Hakuna bingwa wa clean sheet mwisho wa msimu, kuna bingwa wa ligi mwenye pointi nyingi! Focus yetu sisi ni kushinda pointi tatu, hayo mengine ni extra.”
​Kamwe pia ameongeza kuwa wachezaji wote ambao bado hawajapata nafasi kubwa ya kucheza wanaendelea “kupikwa” Avic Town ili waingie vyema kwenye mfumo na mbinu mpya za mwalimu.
​Je, unaikubali kauli hii ya Ally Kamwe kwamba Yanga ya sasa imetumia 25% tu ya uwezo wake? Dondosha maoni yako!
Shiriki:

Habari Zinazohusiana

Zaidi →

Kocha wa Simba Steve Barker Awasha Moto Mpya

YAMAL: Afikisha mchango wa mabao 20 ndani ya mechi 13