Ruka hadi maudhui
SOKALEO

HIZI HAPA HESABU ZA KOCHA WA YANGA KWENYE MCHEZO WA LEO DHIDI YA SIMBA

Chikao
HIZI HAPA HESABU ZA KOCHA WA YANGA KWENYE MCHEZO WA LEO DHIDI YA SIMBA

Kuelekea mchezo wa Ngao ya Jamii kati ya Yanga SC mabingwa wa NBC Premier League vs Simba SC, mabingwa wa CRDB Federation Cup 2025/26 makocha wa timu zote wametamba kutwaa taji hilo.

Watani hawa wa jadi wanatarajiwa kushuka Uwanja wa New Amaan Complex, Agosti 12,2026 ikiwa ni Ishara ya ufunguzi pazia la NBC Premier League msimu mpya wa 2026/27.

Kocha Mkuu wa Yanga SC, Manqoba Mngqithi amesema licha ya kutokuwa na maandalizi ya kutosha kwa msimu mpya anaamini timu yake ina ubora wa kutosha wa kushinda mchezo dhidi ya Simba.

“Mashabiki watafurahi na watarajie soka safi kwa kuwa nina amini katika ubora wa wachezaji na mazoezi ambayo tumefanya. Kikubwa ambacho tunahitaji ni matokeo mazuri na kushinda Ngao ya Jamii.

“Nina miaka 25 katika ukocha, sijawahi kusumbuliwa na presha ya mechi za aina hii, nina uzoefu wa kuhimili presha. Kikubwa ni soka safi na kupata matokeo mazuri,” amesema Mngqithi.

Shiriki:

Habari Zinazohusiana

Zaidi →