Simba SC Leo itakuwa kwenye Uwanja wa Meja Jenerali Isamuhyo kwa mchezo wake wa kwanza wa nyumbani msimu huu dhidi ya Coastal Union, huku macho yakiwa kwa mshambuliaji Ibrahim Doumbia kusubiri kuona kama atafunga bao lake la kwanza.Doumbia amecheza michezo miwili kati ya mitatu hadi sasa, akitumia dakika 113 uwanjani bila kufunga bao, hali ambayo imeanza kuzua mjadala kuhusu kiwango chake.
Kocha wa zamani wa Simba, Dimitar Pantev, amesema bado ni mapema kumhukumu mshambuliaji huyo, akieleza kuwa ana vitu vinavyomuonyesha kuwa ana uwezo wa kuwa mshambuliaji mzuri.Pantev amemtaka Doumbia kutokubeba presha inayotoka nje ya uwanja, akisisitiza kuwa anatakiwa kuwa mtulivu na kuendelea kufanya kazi.
“Anatakiwa kujisaidia mwenyewe, asifanye kosa la kuivaa presha ya nje ya uwanja. Atulie uwanjani, mabao yatakuja.”Pantev pia amesema Doumbia yupo katika timu yenye viungo wazuri ambao wanaweza kumsaidia kupata nafasi na kuonyesha uwezo wake zaidi kadri anavyoendelea kuzoea kikosi.