Mashabiki wa Simba mnaorumbana kwenye vyombo vya habari wote mnahoja za msingi na wote mko sahihi kwa mitazamo yenu
Agizo langu : Ni wote kuacha mara moja marumbano hayo ili kuipa klabu utulivu iendelee kupambana na ligi kuu
Kama mnafanya kwa matakwa yenu basi sitisheni kuanzia sasa na kama ni maagizo basi waambieni wanaowatuma watoke hadharani wazungumze wenyewe ili Dunia ijue wanagombania nini?
Kwa sasa Wana Simba wote tuunganishe nguvu ya pamoja kupambana na maadui 15 wa ligu kuu ya NBC
Tunachokihitaji ni furaha na furaha yetu ni USHINDI!!
MSEMAJI WA TAASISI NIMEAGIZA!! @ahmedally_