Yanga SC na Simba SC zimekata tiketi rasmi ya kushiriki michuano ya CAF Champions League msimu ujao baada ya kuhakikisha zinamaliza msimu katika nafasi zinazowapa uwakilishi wa Tanzania kwenye mashindano hayo makubwa barani Afrika.
Licha ya kufuzu kwao, mbio za ubingwa wa Ligi Kuu Tanzania Bara msimu wa 2025/26 bado zinaendelea, huku bingwa wa msimu huu akiwa hajajulikana rasmi.
Kwa upande wa Simba SC, timu hiyo inaendelea kupambana kuhakikisha inamaliza msimu kwa mafanikio baada ya kukosa ubingwa wa ligi kwa misimu minne mfululizo.
Wekundu hao wa Msimbazi wanatajwa kuwa na hamu kubwa ya kutwaa angalau taji moja muhimu msimu huu.Mashabiki wa soka nchini sasa wanaendelea kusubiri kuona nani atanyakua ubingwa wa ligi huku Yanga na Simba tayari wakijiandaa kwa changamoto za kimataifa msimu ujao.